Vikosi vya usalama Afghanistan
Takriban watu sita na wanamgambo wote wanne wameuawa kwenye mapigano katika jengo la kituo kimoja cha runinga kilicho mji wa Jalalabad nchini Afghanistan.
Wanne kati ya watu waliouawa walikuwa wafanyakazi wa kituo cha RTA. Polisi wawili pia waliuawa.Wengine waliingia ndani na kupambana na vikosi vya usalama kwa muda wa saa nne.
Kundi la Islamic State limedai kuhusika kwenye shambulizi hilo, ambalo lilitokea karibu na ngome ya IS kwenye mpaka na Pakistan.
Wanamgambo wa Taliban pia wako eneo hilo lakini wanasema kuwa si wao walihusika.
Comments
Post a Comment