Bi Park alifikishwa mahakamani akiwa amefungwa pingu
Rais wa zamani wa Korea Kusini, Park Geun-Hye amefikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza mjini Seoul kwa tuhuma za ufisadi.
Hii ndio mara ya kwanza ameonekana hadharani tangu kuondolewa madarakani na kuzuiliwa mwezi Machi mwaka huu. Amekanusha kufanya makosa yeyote.Alipofika mahakamani Park Guen-Hye aliulizwa ajira yake na kujibu hana hajaajiriwa.
Yeye na rafiki wake huyo hawakuzungumziana na walikaa kando ya mawakili wao. Rais huyo wa zamani alivalia mavazi meusi na siyo sare za wafungwa ambazo amekua akivalia gerezani.
Comments
Post a Comment