KUHUSU BONGO MOVIE KUONGWA NA WANAUME...RAIS WAO AFUNGUKIA KAULI YA AUNTY EZEKIEL

 
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania ‘TAFF’, Simon Mwakifwamba.

RAIS wa Shirikisho la Filamu Tanzania ‘TAFF’, Simon Mwakifwamba amempongeza msanii wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel baada ya hivi karibuni kuandikwa kwenye mitandao mbalimbali kwamba sanaa hailipi hivyo wasanii wa kike wanaishi kwa kupewa fedha na wanaume zao.
Akistorisha na paparazi wetu, Mwakifwamba alisema kauli hiyo aliyotoa Aunt ni ukweli mtupu kwani kwa Tanzania sanaa hailipi hivyo wasichana wengi wanaishi kutokana na fedha wanazopata kwa mabwana zao ndiyo maana unakuta wanatembelea magari ya kifahari mpaka watu wanajiuliza wanapata wapi. 
 
Msanii wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel.
 “Alichokisema Aunt ni kweli kabisa na mimi nilishaongea sana kuhusu wasanii wa kike kuuza sura kwa ajili ya kupata mabwana hata Steve Nyerere alishakiri kwamba kwenye tasnia kuna wanaume wanajihusisha na ushoga, sanaa ngumu jamani,” alisema Mwakifwamba.

Comments