Staa wa filamu Bongo, Baby Joseph Madaha amemwagana na aliyekuwa mwandani wake ambaye pia ni meneja wake, Joe Kairuki pasipokuwa na sababu za wazi.
Chanzo chetu cha kuaminika kilichoomba hifadhi ya jina lake kimetutonya kuwa, Madaha na Joe wamebaki kuwa mtu na bosi wake ila msanii huyo sasa amejiweka kwa mwanaume mwingine.
Katika kujua ukweli wa ishu hiyo, mwandishi wetu alimpigia simu Madaha ambaye alisema: “Hee unaniuliza kuhusu Joe, mbona umechelewa kujua? Nimeachana naye, sasa nimejipatia mpenzi wangu mwingine na tunapendana kupita maelezo.”
Comments
Post a Comment