TETESI SAMATTA KUONDOKA FENERBAHCE

Vyombo vya habari nchini Uturuki vinaripoti kuwa Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta anaweza kuondoka katika klabu yake ya Fenerbahce baada ya benchi la timu hiyo kutoridhishwa na kiwango chake tangu atue klabuni hapo kwa mkopo akitokea Aston Villa baada ya kucheza mechi 23 na kufunga magoli 4 tu kwenye ligi kuu ya Uturuki.

KRC Genk ya Ubelgiji ndio klabu pekee inayohusishwa na kumhitaji Mbwana Samatta katika dirisha la usajili mwezi Juni 2021.

Comments