Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imemtoza fainali ya shilingi 500,000, Afisa Mhamasishaji na Msemaji wa klabu ya Yanga Antonio Nugaz.
kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi ya ligi,Nugaz ametozwa faini hiyo kwa kosa la kufanya mahojiano na wanahabari ndani ya eneo la kuchezea wakati wa mchezo wa Gwambina FC dhidi ya Yanga ambao ulimalizika kwa suluhu.
Kwa upande mwingine katika mchezo Namba 76 kati ya Simba SC dhidi ya Mwadui FC ambao ulimalizika kwa Simba kushinda 5-0, kocha Khalid Adam, amefungiwa mechi mbili kuongoza timu yake kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na kwenye benchi la ufundi kwa kukataa mahojiano na wana habari.
Katika mchezo namba 79, kati ya Biashara United dhidi Yanga SC, klabu ya Yanga imetozwa faini ya shilingi 500,000 kwa kosa la mashabiki wao kuwapiga na kuwarushia mawe waamuzi wa mchezo wakati wakielekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Comments
Post a Comment