SIKU chache baada ya staa wa muziki wa Bongo Fleva Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Mungu Yuko Wapi, mashairi ya wimbo huo yamedaiwa kumponza.
Nay aliachia wimbo huo Juni 11 mwaka huu, ambao uliwavuta watu wa kada mbalimbali kuutafsiri kuwa msanii huyo amefanya kufuru kutokana na mashairi kudaiwa kumkosoa Mwenyezi Mungu.
MASHAIRI YA NAY HAYA HAPA
‘Nilizaliwa peke yangu na nitakufa peke yangu, muamini Mungu wako, nibaki na imani yangu,‘Kama kweli kuna mbingu, basi nina njia yangu, Sio baba sio mama basi nitakwenda peke yangu.
‘Hivi kweli huyu Mungu yupo na huu mchafuko, uliowakataza wametawala hivi kweli Mungu yupo?‘Hiyo ni baadhi ya mistari aliyoandika Nay katika wimbo wake huo”.
MASHABIKI WAMJIA JUU
Hata hivyo, mashabiki wa msanii huyo, walimjia juu kutokana na mashairi hayo, na kuhoji kuwa inakuwaje anamkufuru Mungu kiasi hicho, wakati mafanikio yake aliyonayo ni Mungu ndiye alimsimamisha?“Hata kama yanatokea majaribu, ambacho kilitokea miaka ya nyuma.
“Kuna mtu mmoja alikwenda kwa Sheikh ili aelezwe aliko Mungu na apelekwe anakoishi hali ambayo iliibua hisia kali kwa wanafunzi wa Sheikh na kutishia kumuua.
“Unajua hawa wanaojiita wasanii hawakujulishwa kuhusu Mwenyezi Mungu, huyo aliyeimba hivyo anatakiwa ajue kuwa Mungu yupo lakini haonekani, watu kama hawa wanaoimba hivyo wanatakiwa wapewe elimu kwani madhara yapo, na yanaweza kumtokea yule mwenye kumkosoa Mwenyezi Mungu kwa kiburi chake na kutumia ulimi wake,’’ alisema Sheikh Kipozeo.
Naye mtumishi mmoja wa Mungu ambaye aligoma kutajwa jina lake alisema licha ya kwamba Mungu alimpa mafanikio Nay wa Mitego, ni moja ya mapito ambayo Mungu huwapitisha wanadamu, asingepaswa kuweka mashairi ya aina ile” alisema mmoja wa mashabiki zake katika mtandao wa instagram.
VIONGOZI WA DINI WACHARUKA
Baada ya wimbo huo kutoka na kusikilizwa, mbali na waumini wa dini tofauti kuja juu na kumvaa Nay wa Mitego, viongozi wa dini hawakuwa nyuma kutoa dukuduku lao. Viongozi hao walidai kuwa Nay amekosea kuweka mashairi ya aina hiyo kwani yanadhihirisha kumkashifu Mwenyezi Mungu.
Kiongozi wa dini ya Kiislamu anayejulikana kwa jina la Sheikh Hilal Kipozeo, amefunguka na kufafanua kwa kutumia kisa kimoja sasa anamkejeli.
“Ulijaribu kuwasilisha ujumbe lakini uwasilishaji na uimbaji umekosea, kwa sababu Mungu halaumiwi, Ney wa Mitego umekufuru kwa kushindwa kushukuru Neema ulizonazo na vipi zikiondoka, hata muziki wenyewe hutoweza kuimba,’’ aliandika hivyo.
NAY AFUNGUKA
Akizungumzia ishu hiyo ambayo imekuwa ni gumzo katika mitandao na vyombo vya habari, aliendelea kusisitiza kuwa watu wasikilize ujumbe.“Watu wanatakiwa wasikilize ujumbe uliomo ndani, wajue nini kimeimbwa mimi sijakufuru, kama wanavyosema,’’ alisema Nay wa Mitego
Comments
Post a Comment