UONGOZI wa Simba SC umefunguka kuwa sasa kazi imeisha ya kupambania ubingwa wa Ligi Kuu Bara na badala yake wanaangalia namna ya kukijenga kikosi chao kwa ajili ya kushindana Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba tayari imefanikiwa kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2019/20 ikiwa ni mara ya tatu mfululizo, hivyo ina nafasi ya kucheza michuano ya kimataifa iliyo chini ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf).
SIMBA
“Tunatarajia kufanya usajili makini msimu ujao kwani tunahitaji kikosi bora kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ili tuweze kwenda na kasi ya michuano hiyo na kuvunja rekodi ya msimu uliopita kutinga robo fainali.
“Kuna wachezaji ambao wataachwa kwa ajili ya msimu ujao na wapo wale ambao tutawaongeza kutoka sehemu mbalimbali japo mchakato bado haujaanza rasmi na tunasubiria ripoti ya kocha Sven (Vandenbroeck) ndipo tuanze mchakato huo,” alisema Kashembe.Simba imetwaa ubingwa ikiwa imefikisha pointi 79 katika michezo 32 iliyocheza huku ikiwa imebakisha mechi sita.
Comments
Post a Comment