Ukarabati ofisi ya DC Kwimba wafikia zaidi ya asilimia 90


Katibu Tawala Wilaya ya Kwimba Nyakia Chilukile akizungumza na waandishi wa habari mbele ya ofisi ya mkuu wa wilaya ambayo inakarabatiwa kwa sasa.


Katibu tawala Wilaya ya Kwimba akionyesha sehemu ya ofisi ya DC iliyokarabatiwa.Muonekano wa jengo la Mkuu wa Wilaya kwa sasa Mara baada ya ukarabati.


Jumla ya fedha kiasi cha shilingi Milioni  70 zimetumika kukarabati ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza kati ya Milioni 105 zilizoombwa serikalini kupitia Force akaunti.
Hayo yameelezwa na Katibu tawala wa Wilaya Kwimba  Nyakia Ally Chilukile Wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya miradi mbalimbali iliyofanywa na Rais Dkt .John Magufuli Kupitia Force Akaunti.

Das Nyakia anasema Kuwa  jengo hilo ambalo lilikuwa limechakaa na kupoteza muonekano  limekamilika kwa asilimia90 mpaka sasa.

“Mimi Binafsi napenda kumpongeza Rais kwa maoni yake kwani imekuwa inakuja fedha ndogo lakini inafanya kitu kinaonekana “anasema Nyakia

Anasema kuwa mbali na ofisi ya Mkuu wa Wilaya pia wameweza kukarabati makazi ya Mkuu wa  Ambayo yanajengwa kisasa zaidi kuliko ilivyokuwa hapo a wali.

Anataja kuwa katika fedha hizo mpaka sasa wamekwisha pokea kiasi cha fedha Milioni 70 kwa ajili ya ukarabati ofisi ya Mkuu wa Wilaya na kiasi cha milioni 60 kwa ajili ya ukarabati wa jengo la makazi ya DC.

Anaweka wazi licha ya kuomba fedha zaidi ya milioni 105 za ukarabati lakini no milioni 70 tu zimetumika kukarabati hivyo fedha zitakazo ongezeka zitatumika kwa ajili ya kununua Samani za ofisini na vitendea Nazi kama kompyuta na vitu vingine.

Kwa upande wake afisa tarafa wa Wilaya ya Kwimba Hamza Hamza amesema kuwa mradi huo ulianza mwezi may mwaka huu hivyo umetumia miezi miwili tu.

Comments