Tundu Lissu asema atarejea Tanzania Julai 28

HABARI ZA HIVI PUNDE
Mwanasiasa wa upinzani nchin Tanzania Tundu Lissu amesema anatarajia kurudi nchini humo Julai 28.
Tundu Lissu - Wikipedia
Lissu ametangaza nia ya kugombea urais kupitia chama chake cha CHADEMA Oktoba mwaka huu. Mwanasiasa huyo kwa sasa yuko ughaibuni ambapo alienda kupata matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi mwaka 2017.

Akizungumza leo katika mkutano wa njia ya mtandao ulioandaliwa na taasisi ya The Resistance Bureau, Lissu amesema ameshakata tiketi ya ndege na watanzania watarajie kumpokea Julai 28.

Taarifa zaidi kukuijia punde...

Comments