Tunda :Nina Alegi ndo Maana Nina ‘Vipele’ Miguuni

Tunda amfungukia anayedaiwa Bwana'ke | MUUNGWANA BLOG
BAADA ya picha zinazomu-onesha kuwa na vipele miguuni kuzua gumzo mitandaoni, video vixen wa kwenye video mbalimbali za wasanii wa Bongo, Anna Kimario ‘Tunda’ ametaja chanzo cha vipele hivyo.

Tunda alisema kuwa vipele alivyovipata mguuni, vimetoka na ‘aleji’ aliyoipata kwenye samaki, lakini anashangaa watu kumjadili kupita kiasi mitandaoni.

“Kinachonishangaza mtu anasambaza kabisa picha yangu ikionyesha miguu yangu ina makovu, kwani hapo kuna shida gani au kuwa na makovu kwangu sistahili, na ukweli kwamba nilipata aleji ya samaki na hata sio mara ya kwanza kunitokea, niacheni jamani,” alisemaTunda.
Tunda Afungukia Tetesi za 'Kuliwa' na Diamond - Ghafla! Tanzania

Comments