Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 06.07.2020: Havertz, Messi, Saint-Maximin, Bellerin, Alcantara

Lionel Messi
Lionel Messi akifanya mashambulizi

Manchester City huenda ikamsajili mshambuliaji maarufu wa Argentina Lionel Messi, 33, mkataba wake na Barcelona utakapomalizika msimu ujao ikiwa Guardiola ataondoka klabu hiyo. (Talksport)

Chelsea wanapania kuwauza wachezaji wao sita kufadhili uhamisho wa kiungo wa kati wa Ujerumani Kai Havertz, 21, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa karibu euro milioni 90 na klabu ya Bayer Leverkusen. (Express)

Arsenal na Napoli wanamtaka winga wa Newcastle Mfaransa Allan Saint-Maximin, 23. (Le10 Sport in French)

Saint-Maximin
Arsenal na Napoli wanamng'ang'ania winga wa Newcastle Saint-Maximin

Arsenal wanajiandaa kuanza mazungumzao na mshambuliaji wao Mfaransa Alexandre Lacazette, 29, kuhusu mkataba mpya. (Mirror)

Paris St-Germain wanatafakari uwezekano wa kuwasajili beki wa kulia wa Arsenal na Uhispania Hector Bellerin, 25, ambaye pia ananyatiwa na Juventus na Bayern Munich. (Express)

Kiungo wa kati wa Bayern Munich Thiago Alcantara, 29, anatamani sana kuhamia Ligi Kuu ya England, na tayari Liverpool inalenga uhamisho wa £32m wa kiungo huyo wa kimataifa wa Uhispania. (Mail)

Thiago Alcantara
Kiungo wa kati wa Bayern Munich Thiago Alcantara

Hata hivyo, mkufunzi wa Bayern Hansi Flick, anasema klabu hiyo itaongeza juhudi za kumshawishi mchezaji huyo asiondoke. (Sun)

Mlinzi wa England Danny Rose, 30, anahofia mchezo wake Tottenham umemalizika na japo anatafakari siku zake za usoni kwa kujiunga na si Newcastle kwa mkopo. (Mirror)

Sevilla na Atletico Madrid wanakadiria ofa zitakazotolewa kumnunu kiungo wa kati wa Barcelona na Croatia Ivan Rakitic, 32, ambaye anatarajiwa kuondoka Nou Camp msimu huu wa joto. (Marca)
Ivan Rakitic
Sevilla na Atletico Madrid zinamnyatia kiungo wa kati wa Barcelona na Croatia Ivan Rakitic

Mshambuliaji wa Croatia Mario Mandzukic, 34, hana klabu baada ya kufutilia mbali mkataba wke na klabu ya Qatari ya Al-Duhail. (Goal)

Napoli wanataka kumsajili mfungaji mabao hodari wa Lille mwenye umri wa miaka 21-Mnigeria Victor Osimhen. (Corriere dello Sport in Italian)

Comments