Tetesi za soka Ulaya Jumatano tarehe 01.07.2020: Sancho, Hojbjerg, Ake, Torres
on
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
adon Sancho hatagaraniwa zaidi ya pauni milioni 50
Manchester United haitalipa zaidi ya pauni milioni 50 kwa winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho.
Hatahivyo, klabu hiyo ya Bundesliga inataka ongezeko la pauni milioni 100 kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (Sky Sports)
Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 28.06.2020
Arsenal wanafikiria kumtumia Matteo Guendouzi kama sehemu ya mpango wowote wa kubadilishana msimu huu
Arsenal wanafikiria kumtumia kiungo wa kati Matteo Guendouzi, 21, kama sehemu ya mpango wowote wa kubadilishana msimu huu. (Mail)
Tottenham wanaamini kuwa watampata kiungo wa Southampton Pierre-Emile Hojbjerg,24, msimu huu lakini watapaswa kuwauza wachezaji kwanza. (Telegraph)
Manchester United wanafikiria kumchukua Nathan Ake
Manchester City wana mpango wa kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi anayekipiga katika klabu ya Bournemouth Nathan Ake, 25. Hatahivyo wanaweza kukabiliana na ushindani kutoka Chelsea, ambao wanamtaka mchezaji huyo pia. (Athletic)
Beki wa kulia wa Barcelona Marc Jurado,16, ameondoka katika klabu ya Catalan. Mhispania huyo anajiandaa kujiunga na Manchester United msimu huu(ESPN)
Comments
Post a Comment