Leo jumapili Hotmixmziray iliamua kutembelea Kanisa la Decper Life Bible Church lililopo katika mtaa wa Tukunyema eneo la Bomang'ombe wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro na kuweza kushuhudia jinsi Mchungaji Daudi akiwaponya waumini wake waliokuwa na shida mbalimbali.
Wanakwaya wakiimba
Mchungaji Daudi akiwa madhabauni
Maombezi yakiendelea kanisani
Martha Beno Gwele ni binti wa miaka kumi na tisa ametokea mkoa wa Njombe na kuja Kilimanjaro katika kanisa la Deeper Life Bible Church.
Binti huyu alikuwa na shida ya kuanguka degedege na kusumbuliwa na tumbo kwa muda mrefu toka akiwa darasa la sita mpaka anamaliza kidato cha nne na wazazi wake waliangaika kwa waganga pasipo mafanikio yoyote mpaka alipofika hapo kanisani.
Mwanamama huyu Aziza Hasan Juma ambae alikuwa anasumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na kupelekea kulazwa hospital kwa takribani miezi tisa na aliamua kufanya maombi na kubadili dini na kuwa mkristo na kuokoka kabisa baada ya kupona kabisa katika kanisa la Deeper Life Bible Church .
Neema Muheza mwenye umri wa miaka thelathini na saba anaetokea Moshi ambae alikuwa anasumbuliwa na tatizo la mapafu kujaa maji, tatizo hilo lilimempelekea kulazwa hospitali kwa muda wa miezi nane , Lakini toka amefika katika kanisa la mchungaji Daudi aliweza kupona.
Fred Shirima ni kijana mwenye umri wa miaka ishirini na nane ambae alikuwa anasumbuliwa na tatizo la ulevi uliopitiliza kiasi cha kutengwa na familia .
Comments
Post a Comment