MAKAMISHNA WA ARDHI WATAKIWA KUKUTANA NA TAASISI ZINAZODAIWA KODI YA PANGO LA ARDHI


Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo (kushoto) akiwa katika ofisi ya ardhi mkoa wa Rukwa baada ya kuizindua rasmi jana. Wa pili kulia ni Kamishna Msaidizi wa ardhi mkoa wa Rukwa Swagile Msananga na wa tatu kulia ni Katibu Tawala mkoa wa Rukwa Benard Makali.



Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akielekea kukagua ofisi za ardhi mkoa wa Rukwa baada ya kuizindua jana. Kulia kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt Khalfan Haule na kulia ni Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Rukwa Swagile Msananga.



Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiangalia baadhi ya vifaa vya upimaji vilivyopo katika ofisi ya ardhi mkoa wa Rukwa baada ya kuizindua jana. Kushoto ni mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo na wa pili kulia ni  Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Rukwa Swagile Msananga.



Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akioneshwa baadhi ya sehemu zinazofanyiwa ukarabati katika ofisi ya Baraza la Ardhi la Nyumba la wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Said Mtanda jana.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na wananchi wa Namanyele wilayani Nkasi alipokwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya baraza la ardhi na nyumba la wilaya ya Nkasi jana. Kulia kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo.

Sehemu ya wananchi wa Namanyele wilaya ya Nkasi mkoa wa Rukwa waliojitokeza kumpokea Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alipokwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Baraza la Ardhi la Wilaya na Nyumba la Nkasi mkoani Rukwa jana. 

Comments