Mahakama ya mjini Istanbul, Uturuki hii leo imeanza kusikiliza kesi dhidi ya raia 20 wa Saudi Arabia bila ya washtakiwa hao kuwepo mahakamani, baada ya kuhusishwa na mauaji ya mwandishi habari wa Saudi Arabia, Jamal Khashoggi mnamo mwaka 2018.
Mashtaka hayo yanamshutumu Ahmed al-Asiri, mkuu wa zamani wa Idara ya Ujasusi ya Saudi Arabia na Saud al-Qahtani, mshauri wa zamani mwanamfalme Mohammed bin Salman, kwa kuchochea mauaji yaliyopangwa kwa nia mbaya.
Khashoggi aliuawa ndani ya ubalozi mdogo wa Saudia Arabia mjini Istanbul mnamo Oktoba 2, 2018, alikwenda kwenye ubalozi huo kuchukua nakala ili aweze kumuoa mchumba wake wa Kituruki Hatice Cengiz, ambaye alikuwa anamsubiri nje.
Akitoa ushahidi hii leo, Cengiz aliizungumzia siku hiyo ambapo alipokonywa maisha yake ya siku za usoni. Khashoggi alinyongwa hadi kufa na mwili wake ulikatwa vipande vipande.
Comments
Post a Comment