JE MANYIKA JR ALIKUWA AKIIBEBA SINGIDA UNITED




Aliekuwa golikipa wa Singida United Manyika Jr ambae kwasasa anakipiga Polisi Tanzania .Je akikuwa anaibeba Singida United ambayo kwasasa ipo hatihani kushuka dajara?

TUJIKUMBUSHE HISTORIA FUPI YA KIPINDI YUPO SINGIDA UNITED.

"Golikipa wa Singida United Peter Manyika Jr ameendelea kuonyesha kiwango bora baada ya kucheza mechi saba bila kuruhusu nyavu zake kuguswa akiwa na klabu yake hiyo ambayo imepanda daraja msimu huo.
Mechi ya jana ambayo Singida United walishinda bao 1-0 dhidi ya Lipuli FC, imemfanya Manyika kufikisha jumla ya michezo saba bila kufungwa katika mechi 10 za VPL alizocheza msimu huo wa 2017/18.

Mtoto huyo wa Kocha wa makipa wa Yanga Peter Manyika sasa alifikisha rekodi ya golikipa wa Azam Razak Abarola ambaye hajaruhusu goli katika mechi saba za VPL katika mechi tisa alizochezan hadi  msimu huo ulipoisha.

Manyika tayari amecheza michezo 10 wakati Manula akiwa na mechi tisa huku leo akitarajiwa kucheza mechi yake ya 10 ambayo klabu yake ya Simba itacheza na Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya.
Manyika amejiunga na Singida United msimu huu akitokea Simba ambako alikosa nafasi ya kuchcza mara kwa mara lakini tangu ametua kwenye kikosi hicho cha kocha Hans Van Pluijm amejihakikishia nafasi ya kuanza..."
MLINDA MLANGO PETER MANYIKA 'JUNIOR' ASAINI MKATABA WA MWAKA MMOJA ...
Na KCB walivutiwa na Manyika baada ya kumuona akiidaikia Singida United katika michuano ya SportPesa Super Cup Juni mwaka huu mjini Nakuru nchini Kenya.

Manyika ameidakia Singida United kwa msimu mmoja tu baada ya kujiunga nayo akitokea klabu yake ya kwanza kabisa kihistoria, Simba SC alikoanzia timu ya vijana baada ya kusajiliwa Julai mwaka 2014 kufuatia kung’ara akiwa na timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys. 
Aliondoka Simba SC Julai mwaka 2017 baada ya kuidakia jumla ya mechi 51 za mashindano tofauti, nyingi za kirafiki akifanikiwa kusimama langoni mara 30 bila kuruhusu nyavu zake kuguswa huku akiwa amefungwa jumla ya mabao 34.

KWASASA ANAENDELEA KUITUMIKIA POLISI TANZANIA
Manyika Jr alijiunga na Klabu ya Polisi TANZANIA mwanzoni mwa mwaka huu akitokea KCB ya Kenya kwa kandarasi ya mwaka 1 .

Kolikipa Manyika Jr akiwa na wachezaji wenzake
Akiwa mazoezini


Comments