Aishi Manula Awapoteza Makipa Yanga


AISHI Manula, mlinda mlango namba moja wa Simba, amewapoteza makipa wawili wa Yanga katika kukusanya clean sheet na kuwazidi dakika za kukaa langoni.Kwenye mechi tatu za hivi karibuni, Manula ametoka na clean sheet tatu ndani ya dakika 270, huku Mnata akitumia dakika 180 kwenye mechi mbili na Faruk Shikhalo akitumia dakika 90 bila kutoka na clean sheet.

Kuanzia Juni 24, wakati Mbeya City ikikubali kichapo cha mabao 2-0, Juni 28 wakati Prisons ikilazimisha sare ya bila kufungana mechi zote zilichezwa Uwanja wa Sokoine na alimaliza Julai Mosi, wakati Simba inamenyana na Azam FC, Simba ilishinda mabao 2-0 pale Uwanja wa Taifa na kukusanya clean sheet tatu mfululizo.

Kwa upande wa makipa wa Yanga, Juni 24 wakati Yanga inamenyana na Namungo ililazimisha sare ya mabao 2-2, langoni alikaa Mnata, Juni 27 wakati Yanga ikishinda mabao 3-2 mbele ya Ndanda, langoni alikaa Shikhalo na wakati Yanga ikishinda mabao 2-1 mbele ya Kagera Sugar, langoni alikaa Mnata zote zilichezwa Uwanja wa Taifa.

Comments