Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, amempongeza mchimbaji mdogo wa madini aliyetangazwa kuwa Bilionea mpya leo nchini, mara baada ya kuchimba na kuuza mawe mawili ya madini ya Tanzanite yenye uzito wa Kilogramu 15 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 7.8.
Kushoto ni Bilionea mpya Tanzania Saniniu Laizer na kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo alipopiga simu kwa Waziri wa Madini Dotto Biteko, wakati Serikali ilipokuwa ikikabidhiwa madini hayo, baada ya kuyanunua kutoka kwa mchimbaji mdogo Saniniu Laizer wilayani Simanjiro mkoani Manyara.
“Nampongeza sana huyo Laizer, pamoja na wenzake na hii ndiyo faida ya wachimbaji wadogowadogo na hii ni kudhihirisha kwanba Tanzania sisi ni matajiri, nawapongeza sana wananchi wa Simanjiro kwa kazi nzuri wanazofanya, nawapongeza Waziri wa Madini na Wizara ya Fedha kwa kuamua kuyanunua, Laizer hongera sana na ninajua Laizer sasa ataenda kutafuta mwanamke mwingine, sasa ukatafute na mwanamke wa Kisukuma” amesema Rais Magufuli.
Noma sana
ReplyDelete