Mshambuliaji wa Young Africans David Molinga atajiunga na klabu ya RS Berkane inayoshiriki ligi kuu nchini Morocco mara tu baada ya mkataba wake utakapomalizika mwishoni wa msimu huu.
Kocha wa zamani wa Yanga Mwinyi Zahera anatajwa kuwa nyuma ya uhamisho wa straika huyo wa kimataifa wa Congo na ikumbukwe ndiye aliyemsaini klabuni hapo kabla ya kutimuliwa.
David Molinga akiwa na Aliekuwa kocha wa Yanga Mwinyi Zahera.
"Kila kitu kuhusu uhamisho tayari kimekwisha fanyika na sasa tunasubiri ni mkataba wake na Yanga kumalizika" Zahera akizungumza na Mwanaspoti.
Hadi sasa msimu huu David Molinga ndio kinara wa mabao katika klabu ya Yanga, amefanikiwa kuweka mabao 10 kwenye ligi ya VPL.
Comments
Post a Comment