Jiwe la Bilionea Laizer laibua mapya

Kutoka katika Jamhuri ya watu wa mitandaoni kuanzia Instagram, Twitter, Facebook, na Whatsapp wanasema sasa hivi nchi imepata tajiri mpya na wanawake wanasema wamepata baby mpya ambaye ni Bilionea Saniniu Laizer.

Picha ya kueditiwa ya Msanii wa BongoFleva Malkia akiwa na Bilionea Laizer

Saniniu Laizer ambaye ametangazwa kuwa Bilionea baada ya kuchimba mawe mawili ya madini ya Tanzanite yenye uzito wa Kilogram 15 na  thamani ya Tsh Bilioni 7.8.

Sasa mara baada ya kutangazwa kuwa bilionea Jamhuri ya watu wa mitandaoni wakiwemo mastaa wakaanza mbwembwe zao kuhusu utajiri alioupata Saniniu Laizer ambapo video vixen Tunda amepost picha huku akijipa ubini wa Laizer kwa kuandika "Tunda Laizer".

Kupitia mtandao wa Instagram msanii Malkia Karen yeye ame-edit picha akiwa na Bilionea huyo huku ameandika "Yes Baba, mpaka kifo kitakapotutenganisha maana hata baba mzazi alishakupitisha"

Pia kutoka huko huko mitandaoni Wanawake wengine wanaomba nafasi ya kuolewa na bilionea mara baada ya kutangazwa kuwa atapata pesa hizo.

Aidha kuna picha nyingine inayosambaa mitandaoni ikionyesha ukoo wote wa kabila la kimaasai wakielekea kwa Saniniu Laizer mara baada ya kupata pesa hizo na kuwa bilionea.

Comments