CATALUNYA, Hispania
BEKI wa Liverpool, Virgil van Dijk, amesema kuwa nyota wa Barcelona, Lionel Messi, ni mchezaji hatari zaidi ndani ya kikosi hicho ambacho watakutana nacho leo ndani ya Uwanja wa Camp Nou.
Beki huyo ambaye ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Ligi Kuu ya England, aliwahi kucheza dhidi ya Barcelona miaka sita iliyopita akiwa na Celtic na kuambulia kichapo cha mabao 6-1 ndani ya uwanja huo.
Lakini katika mchezo huo waliokutana Messi hakucheza kabisa sababu ya kuwa majeruhi, lakini hii itakuwa mara ya pili kwa Van Dijk kurudi Camp Nou lakini ni mara ya kwanza atakuwa na kazi ya kumzuia Messi.
“Mara zote huwa nasema Messi ni mchezaji bora duniani, tunajua uwezo wake, hii itakuwa mara ya pili kucheza Camp Nou lakini itakuwa tofauti na wakati ule.
“Hatuchezi kwa kumzuia mchezaji mmoja, kama umegundua tumekuwa tukifanya kazi wote ya kushambulia na kuzuia,” alisema beki huyo raia wa Uholanzi.
Comments
Post a Comment