Nape Nnaye, Godbless Lema, MO Dewji na wengineo kuhusu kifo cha Dkt. Reginald Mengi Muungwana Blog 3 Thursday, May 02, 2019


Watu mbalimbali wamezidi kutuma salamu za pole kufuatia kifo cha Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi kilichotokea usiku wa kuamkia leo. Chini ni baadhi ya  viongozi waliotuma salamu zao za pole kupitia mitandao.

Nape Nnauye - Umeacha alama kubwa! Nimejifunza mengi kwako, Rafiki, Mshikaji, Kiongozi na Mzazi! Ulinifundisha kuwa KUKATA TAMAA NI DHAMBI! {Msalimie Mzee Sitta, mkumbushe kile kikao chetu Cha mwisho nyumbani kwako}Pumzika kwa Amani Dr. R.A Mengi.

Godbless Lema - Watu wanagopa kifo,kimsingi tunacho ogopa ni kuwahi kufa kwani kifo hakizuiliki,ktk maisha ni vyema kuishi maisha ya baraka na watu wote,ili utakapo tangulia maisha yako yaweze kuwa na thamani.Nina mshukuru Mungu kwa ajili ya maisha ya Dr R.Mengi,kwani alijua thamani ya ubinadamu

January Makamba - Pole kwa Jacqueline na Regina, Abdiel and the twins - na familia nzima ya IPP Group. Mungu ailaze roho ya Mzee Reginald Mengi peponi.

Prof. Jay - R.I.P Mzee Mengi, Umeacha Alama kubwa sana kwenye jamii yetu, Tangulia Nasi tunafuatia.

Mohammed Dewji MO - Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un. Mwenyezi Mungu ampe pumziko na ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Ameen 🙏🏽 #RIPMengi

Halima Mdee -  Nimepokea kwa Masikitiko MAKUBWA SANA kifo cha Ndugu Reginald Mengi. Nawapa POLE sana FAMILIA,JAMAA na Marafiki. Mwaka 2019 unaendelea kuwa wa MAJONZI kwetu kama TAIFA,TUNAPOTEZA watu MAKINI waliokuwa na MCHANGO mkubwa SANA katika ujenzi wa NCHI yetu.Upumzike kwa AMANI Mkuu.

Joseph Kusaga - R.I.P mzee wangu... #ReginaldMengi 😔. This has been a trauma year for our media industry..

Msemaji Mkuu wa Serikali (Dkt. Abbas) - Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mwenyekiti wa IPP, Mzee Reginald Mengi. Kama alivyopata kusema yeye mwenyewe siku za uhai wake kuwa watu wanaoacha alama hawafi, basi mawazo, falsafa, ubunifu na kujitoa kwake vitaendelea kuishi nasi.

Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi amefariki dunia, kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo vya habari alivyokuwa anavimiliki. Mengi ambaye ni mmoja kati ya wafanyabishara wakubwa Tanzania amefariki usiku wa kuamkia leo Alhamisi akiwa Dubai.

Comments