Waendesha mashitaka nchini Sweden wamefungua upya kesi ya ubakaji dhidi ya mwanzilishi wa mtandao wa uvujishaji wa nyaraka za siri Wikileaks, Julian Assange baada ya kuondolewa kwenye ubalozi wa Ecuador mjini London, Uingereza.
Waendesha mashitaka walifungua mashitaka ya mwanzo dhidi ya Assange alipoitembelea nchi hiyo mwaka wa 2010. Miaka saba baadaye, kesi ya madai ya ubakaji ikafutwa baada ya muda wa kuiendesha kesi hiyo kumalizika.
Comments
Post a Comment