Mfalme Akihito wa Japan ang’atuka madarakani, amuachia kiti cha uongozi mwanawe, ni baada ya utawala wake wa miaka 30
Mfalme Akihito ametangaza kuachia madaraka katika hotuba yake ya mwisho, rasmi kwa watu wa taifa lake huku akiwashukuru Wajapani kwa msaada wao wakati wa utawala wake wa miaka 30 ulioshuhudia mafanikio na changamoto.
Mfalme alifanya maombi mbele ya Mungu wa Jua “Shinto” siku ya Jumanne (Aprili 30), huo ukiwa ni mwanzo wa hatua za kumalizika kwa utawala wake wa miaka 30. Mfalme huyo mwenye umri wa miaka 85 alivaa vazi la kijadi alipokwenda Hekalu la Kashikodokoro kuielezea miungu kuhusu kustaafu kwake.
Akihito ndiye wa kwanza wa Japan kuachia madaraka katika muda wa karne mbili. Alisema ilikuwa ni heshima kubwa kwake kutekeleza majukumu yake huku watu wa Japan wakiwa na imani kamili kutokana na uongozi wake.
Mfalme Akihito atamwachia mamlaka mwanawe Naruhito.
Korea Kusini yamshukuru
Mfalme wa Japan anayeondoka Akihito na mkewe Malkia Michiko (picture-alliance/dpa/N. Datiche)
Mfalme wa Japan anayeondoka, Akihito, na mkewe, Malkia Michiko
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kusini, Kim In Chul, alisema Rais Moon Jae-In amemshukuru Mfalme Akihito kwa kuweka msisitizo juu ya amani na mchango wake juu ya kuendeleza mahusiano mema kati ya Korea ya Kusini na Japan na kwamba alitarajia kuwa mfalme huyo angeliendelea kuunga mkono maendeleo na mahusiano ya nchi hizo mbili hata baada ya kustaafu kwake.
Msemaji huyo wa wizara ya mambo ya nje pia alisema serikali ya Korea Kusini pia ilimpongeza mfalme mpya, Naruhito, na kuongeza kwamba Korea Kusini inatarajia mahusiano mazuri kati ya nchi mbili hizo yangeliendelea.
Katika sherehe zilizotarajiwa kufanyika kwenye kasri baadaye Jumanne, Mfalme Akihito alitazamiwa kutangaza rasmi kustaafu kwake mbele ya viongozi wa serikali na wana familia ya kifalme.
Hata hivyo, mfalme huyo angeliendelea kuwa mtawala hadi saa sita usiku kwa saa za Japan, ambapo mwanawe, Mwana Mfalme Naruhito, angelirithi kiti cha enzi siku ya Jumatano (Mei Mosi) na kuwa mfalme mpya.
Katika sherehe tofauti, Naruhito pia alitazamiwa kurithi vitu vya utawala wa kifalme kama mavazi, upanga, vito na mihuri ya kifalme.
Kama baba yake, Naruhito alitarajiwa kuwa na ushawishi wa kisiasa katika utawala wa kifalme badala ya kung’ang’ania mila za Kijapani.
Mwana Mfalme huyo alipata elimu yake katika Chuo Kikuu cha Oxford cha Uingereza na amemuoa Masako Owada aliyesoma katika vyuo vikuu vya Harvard na Oxford.
Wote wawili wana uzoefu wa kimataifa unaotarajiwa kuleta chachu mpya katika taifa la Japan.

Comments
Post a Comment