Liverpool kunyakua Ubingwa kesho?


Kesho klabu ya  Liverpool itamaliza mchezo wake wa mwisho wa Ligi Kuu England kwa kumenyana na Wolves mchezo utakaopigwa uwanja wa Anfield.

Liverpool wana pointi 94 wakiwa nafasi ya pili kwenye msimamo huku wapinzani wao Manchester City wakiwa nafasi ya kwanza na wana pointi 95 kesho watamenyana na Brighton ugenini.

Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa atatazama mchezo wake kwa ukaribu kabla ya kusubiri matokeo ya mpinzani wake.

"Ni mchezo wetu wa fainali ni lazima tuonyeshe kwamba tunahitaji kupata matokeo kwa nguvu na ushirikiano.

"Haitakuwa kazi nyepesi kupata matokeo ila nia ipo na tumewekeza nguvu nyingi kwenye mchezo wetu wa mwisho," amesema.

Comments