LICHA ya kwamba Shiza Kichuya na Himid Mao wapo nchi ya ugenini huko Misri, lakini itabidi waweke udugu pembeni kesho kwa dakika 90 kila mmoja akitetea timu yake.
Kichuya ambaye anaichezea ENPPI, ndio watakaokuwa wenyeji wa Petrojet, ambayo anachezea Himid Mao, kila timu ikitaka kushinda ili kujisogeza nafasi nzuri kwenye msimamo.
Kikosi hicho cha ENPPI anachochezea Kichuya hakipo nafasi nzuri sana kwenye msimamo, kwani kina pointi 30, kikiwa nafasi ya 15 kati ya timu 18 zinazoshiriki ligi hiyo, hivyo leo kinataka kushinda ili kujinasua nafasi hiyo.
Kwa upande wao Petrojet ya Himid Mao, wanashika nafasi ya 13, wakiwa na pointi 34 katika michezo yao 30 waliyokwisha kucheza, nao wakitakiwa kupambana wasishuke daraja.
Kichuya amesajiliwa na Pharco FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini humo na anacheza kwa mkopo Klabu hiyo ya ENPPI iliyopo Ligi Kuu
Comments
Post a Comment