Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wawili, Abraham Nsajigwa (37) na Festo Zakaria (35) Kwa tuhuma ya kupatikana mali ya wizi gari lenye namba ya usajili T.899 DCW aina ya Noah rangi nyeusi.
Watuhumiwa wamekamatwa mnamo Mei 12 mwaka huu majira ya 02:00 usiku huko maeneo ya Isanga, Kata ya Isanga, Tarafa ya Sisimba, Jijini Mbeya.
Gari hiyo iliibwa huko Temeke Mkoani Dar es Salaam ambapo baada ya tukio hilo, taarifa zililifikia Jeshi la Polisi na kuanza msako na jana kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wakiwa na gari hilo.
Comments
Post a Comment