LONDON, England
MKUU wa benchi la ufundi la Arsenal, Unai Emery, amewatoa wasiwasi mashabiki wake, akiwaambia watamaliza msimu huu wakiwa top four licha ya kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Leicester City.
Arsenal walikuwa na siku mbaya mbele ya Youri Tielesman na Jamie Vardy aliyefunga mara mbili katika mtanange huo wa Ligi Kuu ya England.
Matokeo hayo yaliwabakiza Gunners katika nafasi ya tano, wakiwa wameachwa pointi mbili na Chelsea wanaoikamilisha orodha ya timu nne za juu.
“Tumesikitishwa lakini tunatakiwa kukumbuka tulivyokuwa miezi mitatu iliyopita,” alisema Emery na kuongeza: “Bado tunaweza kurejea top four.”
Arsenal wamebakiza michezo miwili kukamilisha ratiba ya Ligi Kuu ya England msimu ambayo watacheza dhidi ya Brighton na Burnley.
Comments
Post a Comment