LICHA ya Simba kuwa na kasi kubwa ya kuvitafuna viropo vyao, Meneja wa Yanga, Nadir Haroub `Cannavaro,’ amesema kikosi chake pia kina nafasi ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Yanga inaendelea kuwa kileleni ikijikusanyia pointi 77, baada ya kuwafunga Azam FC bao 1-0, mchezo uliochezwa Jumatatu ya wiki hii Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na DIMBA Jumatano, Cannavaro alisema wanaodhani mbio hizo za ubingwa zinawahusu Simba peke yake watakuwa wanakosea, kwani hata Yanga wana nafasi nzuri ya kuutwaa.
“Hakuna timu yenye uhakika wa moja kwa moja kutwaa ubingwa huu, kwani hatujaachana sana. Sisi ndio tunaoongoza, hivyo mtu akisema hatuwezi kuutwaa anakosea.
“Baada ya kuwafunga Azam wachezaji wetu wamezidi kujiamini na tumeongeza pointi muhimu, hivyo binafsi nadhani mapambano haya yataendelea hadi mwisho,” alisema.
Comments
Post a Comment