Spika Ndugai aeleza kumalizana na Tundu Lissu


Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema mhimili huo wa Dola umeshamlipa madai yake yote mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu huku akimwagiza kuwa kama ana jambo lolote kuwasiliana na mamlaka husika na si kutumia mitandao ya kijamii.

Ndugai alitoa kauli hiyo juzi ikiwa zimepita siku 10 tangu mnadhimu huyo wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kumwandikia barua Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai akimtaka kumlipa mshahara na posho zake za kuanzia Januari, ndani ya siku 14.

Utakumbuka Septemba 7, 2017 Tundu Lissu alishambuliwa na kujeruhiwa vibaya kwa risasi
akitokea Bungeni Jijini Dodoma. Lissu alipatiwa matibabu ya mwanzo nchini Kenya kisha kuhamishiwa Ubelgiji ambapo yupo kwa sasa.

Comments