Simba yatuma malalamiko kwa CAF baada ya kubadilishiwa waamuzi kwenye mchezo wao dhidi ya TP Mazembe
Baada ya Shirikisho la soka barani Afrika CAF kufanya mabadiliko ya waamuzi watakao chezesha mchezo wa marudiano kati ya TP Mazembe dhidi ya Simba ambao utachezwa katika mji wa Lubumbashi nchini DR Congo, Simba wameamua kuwatumia malalamiko shirikisho hilo la soka kwa uamuzi huo walioufanya wa kuwabadilishia waamuzi ambao walikuwa wanatoka katika taifa la Ethiopia na Kenya na badala yake kuwaletea waamuzi wanaotoka kwenye taifa la Zambia na Eritrea.
Ikumbukwe CAF wameamua kubadili waamuzi hao kutokana na sababu ambazo wamesema ni sababu za kiufundi ambazo zimesababisha mabadiliko hayo kufanyia na Simba wametoa malalamiko hayo kwa kudai kwamba ni habari za kushtusha lakini pia CAF wametoa taarifa hizo bila kuwasiliana na uongozi wa Simba na kuwaeleza kiundani kitu ambacho wangetakiwa kufanya hivyo.

Comments
Post a Comment