Nchi ya Rwanda leo hii inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 25 ya mauaji ya Kimbari ambapo watu wapatao 800,000 hasa wa kabila la Watutsi waliuawa.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Deutsche Welle (DW), Wajumbe kadhaa wa Kimataifa waliwasili jana siku ya Jumamosi katika mji mkuu, Kigali kwa ajili ya kuhudhuria kumbukumbu ya mauaji hayo ya Kimbari.
Mnamo Aprili 7 mwaka 1994, mauaji ya Kimbari yalianza katika taifa hilo la Afrika Mashariki na kuendelea kwa siku 100.
Rais wa Rwanda Paul Kagame na wageni wa heshima wataweka mashada ya maua kwenye eneo maalum la kumbukumbu ya mauaji hayo ya Kimbari mjini Kigali.
Maadhimisho yatafanyika katika uwanja wa michezo wa mji huo mkuu ambapo Rais wa Tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker anatarajiwa kuwepo.
Serikali ya Ufaransa imesema itawakilishwa na mwanasiasa Herve Berville, manusura wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda. Berville ni yatima aliyekwenda Ufaransa mwaka 1994.
Comments
Post a Comment