Maurizio Sarri akubali yaishe kwa Hazard ‘Chelsea haina uwezo tena wa kumzuia, pauni milioni 100 ni ndogo sana’

Kocha Maurizio Sarri amesema kuwa dau la pauni milioni 100 kwa Eden Hazard ni dogo mnoo lakini hakuna namna maana Chelsea haina uwezo tena wa kumzuiya.


Hazard amehusika kwenye mabao yote mawili ya Chelsea iliyotoka na ushindi wa 2 – 0 dhidi ya West Ham na kuifanya timu hiyo kutinga nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Premier League muda mchache tu tangu taarifa kuenea kuwa Real Madrid inakaribia kumnasa mchezaji huyo usajili wa kipindi cha majira ya joto.

Sarri amesema kuendelea kumzuia Hazard itakuwa ngumu kwa sasa, lakini anaamini thamani yake ni zaidi ya kiasi hicho cha pauni milioni 100.

” Pauni milioni 100 ni kiasi kidogo mno katika soko hili la usajili. Tumeona dirisha la usajili lililopita thamani za wachezaji zilivyokuwa, hivyo naamini kupata mbadala wa Hazard ni ngumu.” amesema Maurizio Sarri.

Alipoilizwa uwezo wa klabu wa kumzuia mchezaji huyo muhimu Hazard kutoondoka, Sarri amesema “Siwezi kufanya kitu chochote kitakachomfanya aenele kubaki, kwa sababu nimeshafanya makubaliano na klabu, Eden anataka kupata changamoto mpya hivyo ni vigumu kuendelea kumshikilia.”

”Lazima tuheshimu maamuzi yake lakini kama ningekuwa mmiliki wa klabu au mmoja kati ya wajumbe wa bodi ningeliingilia kati swala hili na angalau kumshauri hata kidogo kuona kama ningeweza kubadili mawazo yake.”

Comments