Leo April 9, 2019 kutoka katika ukurasa wa Twitter wa Waziri wa Maliasili na Utalii Dr. Hamis Kigwangalla ametoa ushauri kwa Viongozi vijana waliopewa nafasi katika Serikali au Vijana walioweza kupata fedha .
Ameandika >>> “Kuna vijana wakipewa madaraka ama wakitajirika basi hubadilisha tembea/sema yao, dharau inatamalaki na hata husahau walikotoka. Katika maisha yangu mafupi kwenye siasa za kitaifa nimewashuhudia wengine hata wakijiona wakubwa kuliko wakubwa zao. Nawasihi wajifunze kwa Luqman!”
Comments
Post a Comment