Mchezaji wa Timu ya Simba SC, Jonas Mkude ametoa fedha taslimu shilingi laki tano kumsaidia mchezaji wa zamani wa Pamba ya Mwanza na Simba, Alphonce Modest kwa ajili ya matibabu.
Modest ambaye amezichezea timu za Yanga SC na Mtibwa Sugar, amekuwa akisumbuliwa na homa kwa muda mrefu.
Pia wachezaji wa zamani kupitia Chama chao wametoa shilingi laki saba kumchangia mwenzao, Fedha hizo zimekabidhiwa kwa baba yake Modest mitaa ya Kinondoni jijini Dar Es Salaam.
Comments
Post a Comment