Baada ya kumaliza adhabu ya kukosa mechi tatu za Ligi Kuu Bara, beki aliyechukua jezi ya Nadri Haroub Cannavaro, Abdallah Shaibu maarufu kama Ninja, leo anatarajiwa kuwa sehemu ya mchezo wa ligi kati ya Yanga dhidi African Lyon.
Ninja amemaliza adhabu hiyo aliyoipata kutokana na kumchezea rafu mbaya mchezaji wa Coastal Union kwa kumpiga kiwiko katika mchezo wa ligi uliofanyika Mkwakwani, Tanga.
Kumalizika kwa adhabu hiyo kunampa nafasi Ninja ya kuwa sehemu ya mchezo wa leo, Yanga tayari imeshawasili jijini Mwanza takribani siku tatu sasa na tayari kwa mchezo huo ambao utakuwa ni muhimu kwa Yanga ikikumbuka sare ya bao 1-1 walioyoipata baada ya kucheza na Ndanda huko Mtwara.
Comments
Post a Comment