AMUNIKE: SITAISAHAU MECHI YA UGANDA


MECHI ngumu kati ya tano za kufuzu Kombe la Afrika ambazo kocha mkuu wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Emmanuel Amunike, amekumbana nayo tangu akabidhiwe mikoba ni dhidi ya Uganda The Cranes.

Amunike, raia wa Nigeria, alichukua mikoba ya kuifundisha Taifa Stars kutoka kwa Salum Mayanga, ambaye sasa ni kocha wa Mbao FC na kuiongoza timu hiyo kwa mechi tano ambazo ni nyumbani na ugenini dhidi ya Uganda, nyumbani na ugenini dhidi  ya Cape Verde na ugenini dhidi ya Lesotho.

Katika mechi hizo tano, Amunike alishinda mbili ambazo zote ni nyumbani dhidi ya Uganda na Cape Verde, sare ugenini dhidi Uganda na kupoteza ugenini dhidi ya Lesotho.
Image result for amunike

Akizungumza hivi karibuni jijini Dar es Salaam alipotembelewa na hotmixmziray iliyopo kijitonyama, Amunike alisema hataisahau mechi yake ya kwanza ugenini dhidi ya Uganda Cranes, iliyomalizika kwa sare ya kutofungana.
Image result for amunike
Alisema kabla ya mechi hiyo alishapewa historia ya namna Taifa Stars inavyotaabika nyumbani na ugenini ikicheza na Uganda Cranes na kiwango bora walichonacho.

“Hii ilikuwa mechi ngumu kwangu, kwasababu ndiyo kwanza nimekabidhiwa timu na sijawafahamu vizuri wachezaji wangu, ikizingatiwa hata muda wa mazoezi nao ulikuwa mfupi, lakini nashukuru Mungu tuliondoka na pointi moja,” alisema Amunike.

Kocha huyo wa Taifa Stars alisema wamepata pointi nne kutoka Uganda Cranes, ambayo ndiyo ilikuwa timu tishio katika kundi lao na walimaliza wa kwanza, wakiwa wamefuzu Kombe la Afrika, bado hawajacheza mchezo mmoja.

Amunike ameingia katika historia ya soka la Tanzania baada ya kuiongoza Taifa Stars kucheza Kombe la Afrika tangu wafanye hivyo mwaka 1980. Michuano ya mwaka huu itafanyika kuanzia Juni nchini Misri.

Comments