Mwimbaji R. Kelly ametoka gerezani mjini Chicago baada ya mtu ambaye hakutaka kujulikana kumlipia zaidi ya Tsh. Milioni 377 kwa ajili ya malezi ya watoto wake ili mwimbaji huyo aachiwe huru, R.Kelly alirudishwa tena jela baada ya kushindwa kulipa fedha hizo kwa ajili ya malezi ya watoto wake.
Inadaiwa kuwa R.Kelly amekuwa akimtupia lawama aliyekuwa mke wake Andrea na kusema kuwa kutokana na uongo anaousambaza juu ya sakata lake la unyanyasaji wa kingono kwa wasichana wadogo ndio sababu inayomfanya mkongwe huyo kukosa hela za kumpa ili kuwatunza watoto wao.
Inaripotiwa kuwa tokea mwaka 2017 R. Kelly alikata mawasiliano na mzazi mwenzake Andrea pamoja na watoto wake watatu na kubadilisha namba ya simu bila kumpa taarifa yoyote Andrea.
Comments
Post a Comment