Waziri Kigwangala atoa msimamo vita dhidi ya ujangili


Waziri wa Maliasili na Utalii,  Dkt. Hamisi Kigwangala amewataka Watanzania kuondokana na dhana iliyojengeka miongoni mwao kuwa watumishi wa Wizara hiyo hususan  wahifadhi wa  wanyamapori na Misitu  ni watu katili  wanaowatesa Wananchi.

Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua mkutano wa 26 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika katika Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi jijini Mwanza.

Amesema watumishi hao ni watu wenye utu na weledi wa hali ya juu na wanaozingatia  sheria katika kutimiza majukumu yao na hulazimika kutumia nguvu wakati wakipambana na majangili wanaokutwa katika maeneo ya hifadhi wakifanya vitendo vya ujangili.

‘’ Ulinzi wa Rasilimali za nchi ni jukumu letu sote, wizara imepewa dhamana ya kusimamia na kuongoza kwa niaba ya watanzania, kama kuna watumishi wa Wizara hii wanaowanyanyasa wananchi naomba walete ushahidi kwetu ili tuwachukulie hatua’’ amesema Dkt. Kigwangala.

Comments