Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) Tundu Lissu amesema ameandika barua kupitia kwa mawakili wake kwa uongozi wa Bunge, akishinikiza kulipwa mshahara na stahiki zake ndani ya siku 14, lasivyo ataushtaki mahakamani uongozi wa Bunge .
Lissu amesema aliwaagiza mawakili wake kuwasiliana na uongozi wa Bunge ili kufahamu ni lini wataanza kumpatia tena mshahara wake na stahiki za kibunge.
“Mawakili wangu wamemwandikia barua Katibu wa Bunge, Kagaigai ya kumtaka kulipa mshahara na posho zangu za kibunge za tangu Januari mwaka huu. pia walimpa siku 14 kutekeleza madai, vinginevyo tutafungua madai Mahakama Kuu”, amesema Lissu na kuongeza;l
“Bunge halina mamlaka yoyote ya kisheria kuzuia au kukata au kupunguza mshahara wa mbunge na posho zinazotokana na ubunge, isipokuwa tu kama mbunge husika amesimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa azimio la Bunge kutokana na kukiuka maadili ya kibunge.”
“Na hilo haliwezi kufanyika bila kwanza Spika wa Bunge kuielekeza Kamati ya Maadili na Mamlaka ya Bunge kushughulikia suala hilo kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge.”
Machi 14, 2019 Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu aliibua madai ya kutoingizwa mshahara wake na Mhimili wa Bunge madai ambayo Spika wa Bunge, Job Ndugai alijibu kuwa alipaswa kuuliza uongozi wa Bunge juu ya mshahara wake
Comments
Post a Comment