Maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kutoa salamu kwa Ruge Mutahaba aliyegusa nyoyo za wengi ziliongozwa na Rais Dkt.John Magufuli, Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Kikwete aliyeambatana na mkewe pamoja na Waziri mkuu Kassimu Majaliwa na mkewe Mary Majaliwa. Wakati huo huo msanii Naseeb Abul maarufu kama Diamond Platnumz , Fleva Ali Kiba, Mwana FA na Ommy Dimpoz pia waliwasili katika viwanja hivyo kwa ajili ya kutoa salamu za mwisho.
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Ruge Mutahaba ambaye aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumamosi March 2, 2019
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Ali Kiba pamoja na Mwana FA na Ommy Dimpoz wakitoka kuaga mwili wa marehemu Ruge Mutahaba ambaye aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumamosi March 2, 2019.
Msanii wa muziki wa bongo Flava Nasibu Abdul "Diamond Platinumz" akiwasili katika msiba wa marehemu Ruge Mutahaba ambaye aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumamosi March 2, 2019
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Harmonize akiondoka mara baada ya kuaga mwili wa marehemu Ruge Mutahaba ambaye aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumamosi March 2, 2019.
Msanii wa kizazi kipya Barnaba akiondolewa ukumbini akiwa amebebwa baada ya kuishiwa nguvu kutokana na uchungu mkali alio nao.
Mwili wa marehemu Ruge Mutahaba ambaye aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment ukitolewa kwenye ukumbi wa Karimjee mara baada ya kuagwa leo Jumamosi March 2, 2019
Viongozi mbalimbali walijitokeza kutoa heshima za mwisho
Waombolezaji wakiwa kwenye viwanja wakifuatilia kwenye Skrini kinachojiri ndani ya ukumbi
Comments
Post a Comment