TAIFA STARS YAICHAPA UGANDA 3G....WATANZANIA VICHEKO KILA KONA


Dakika 90 za mchezo kati ya Timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda zimemalizika katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kwa Taifa Stars kuifunga Uganda bao 3 - 0.
Mabao ya Stars yalianza kuwekwa kimiani na Simon Msuva dakika ya 21 akimalizia pasi ya John Bocco bao ambalo lilidumu mpaka kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili mapinduzi yalikuwa makubwa ambapo Erasto Nyoni alifunga bao dakika ya 51 akifunga kwa mkwaju wa penati.

Dakika ya 57 Agrey Morris alifunga bao la tatu akimalizia pasi ya Bocco hivyo kufuzu hatua hiyo kwani matokeo ya Lesotho na CapeVerde ngoma droo.
Taifa Stars imefanikiwa kufuzu Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) kwa mara ya pili ikiwa ni maka 39 imepita tangu iingie kwenye michuano hiyo.


Taifa Stars imefuzu kwa ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Uganda, ambapo Matokeo mengine Lesotho imetoa sare ya 0-0 dhidi ya Cape Verde.


Comments