Simba SC Mabilioni ya fedha nje nje


Hapo jana Simba SC walifanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika (CAFCL)
baada ya kuichapa AS Vita kutokea DR Congo.

Kufikia hatua hiyo Simba SC inavuna kiasi cha US Dollar 650,000 (zaidi ya TSh Bilioni 1.5), na sasa inasubiri kujua itapangwa nani katika hatua hiyo inayoshirikisha klabu nane zilizopenya usiku wa jana.

Kama Simba SC itasonga mbele kufikia hatua ya nusu fainali watapokea Tsh Bilion 1.84. Na endapo wakifika fainali watakuwa na uhakika ya kubeba Tsh Bilion 2.87, kama watatwaa ubingwa
huo basi watabeba Tsh Bilion 5.75.

Comments