Mazishi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds, Ruge Mutahaba yamehudhuriwa na vigogo zaidi ya kumi wakiwemo Mawaziri, Wabunge na Wakuu wa Mikoa.
Ratiba iliyotolewa leo asubuhi Jumatatu Februari 4,2019 inawataja baadhi ya vigogo hao ambao ni mawaziri na wizara zao kwenye mabano ni Dk Hamisi Kigwangalla (Maliasili na Utalii), Dotto Biteko (Madini), January Makamba (Muungano mazingira), Angela Kairuki(uwekezaji) na Juma Aweso ambaye ni Naibu Waziri wa Maji.
Pia, wabunge wanaotajwa kwenye ratiba hiyo ni Nape Nnauye (Mtama-CCM), Rudhiwani Kikwete (Chalinze-CCM), Aieshi Hilary (Sumbawanga Mjini- CCM) na wabunge wote wa Mkoa wa Kagera na wakuu wa wilaya.
Wengine ni Wakuu wa mikoa ya Simiyu (Anthony Mtaka), Mwanza (John Mongella), Mara (Adam Malima) na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hoseah Ndagala.
Sanduku lenye mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Marehemu Ruge Mutahaba ukiwa tayari umewekwa katika uwanja wa Gymkana,Bukoba mkoani Kagera kwa ajili ya kuagwa,Ibada na baadae kurejeshwa tena Kiziru kwa ajili ya Mazishi.Katika sughuli hiyo viongozi mbalimbali wa Serikali,ndugu jamaa na marafiki wamefika uwanjani hapo kumpa heshima ya mwisho mpendwa wao.
Sanduku lenye mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Marehemu Ruge Mutahaba ukiwa tayari umewasili katika uwanja wa Gymkana,Bukoba mkoani Kagera tayari kwa kupewa heshima ya mwisho.
Waziri wa Madini, Mhe. Dotto Biteko akiwasili katika viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba asubuhi hii katika ibada ya kumuaga aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi Clouds Media Group marehemu Ruge Mutahaba.
Mkuu wa Mkoa Mara, Mhe. Adam Malima akiwasili kwenye viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba asubuhi ya leo kuhudhuria ibada ya mazishi ya aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi Clouds Media Group marehemu Ruge Mutahaba inayofanyika viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba.
Mtoto wa marehemu Ruge akiweka ua katika kaburi la marehemu baba yake ambaye amezikwa leo kijijini kwao Kiziru Bukoba.Hatimaye mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba umezikwa kishujaa nyumbani kwao katika kijiji cha Kiziru Kata ya Karabagaine Wilaya ya Bukoba na hakuna mahubiri yaliyotolewa na katibu huyo.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga, aakiweka mashada katika kaburi la marehemu Ruge Mutahaba ambaye amezikwa leo kijijini kwao Kiziru Bukoba,Shughuli za maziko zilianza kwa Ibada ya mazishi ambayo iliongonzwa na Katibu wa Parokia ya Itahwa, Anatory Kyatwa huku nyimbo za kihaya zikipamba tukio la mazishi.
Wazazi, familia, wakiweka shada la maua katika kaburi la mpendwa wao,marehemu Ruge Mutahaba ambaye amezikwa leo kijijini kwao Kiziru Bukoba.Katika shughuli hiyo viongozi mbalimbali wa Serikali wameshiriki,wakiwemo wasanii wa Bongo Muvi,Muziki,marafiki,ndugu na jamaa kutoka sehemu mbalimali walitoa heshima yao ya mwisho kwa mpendwa wao Ruge katika Viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba kabla ya kuzikwa kijijini kwao.
Mkuu wa MKoa wa Dar Es Salmaa,Paul Makonda akiweka maua katika Kaburi la Ruge.
Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira, January Makamba akiweka shada.
Awali wakati wa tukio la kuaga mwili wake katika viwanja vya Gymkhana, Maaskofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba walimtaja Ruge kama kijana jasiri mzalendo na mfano wa kuigwa.
Askofu Desderius Rwoma ameitaka jamii kuenzi mambo mema aliyoacha huku msaidizi wake, Methodius Kilaini akisema vijana wengi wamepata mafanikio kutokana na udhubutu wake na ujasiri wa kusimamia anayoamini.
Mbunge wa jimbo la Sumbawanga mjini, Mhe. Aeshi Hillary akisalimiana na mbunge wa jimbo la Kigoma mjini, Mhe Zitto Kabwe katika viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba asubuhi hii katika ibada ya kumuaga aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi Clouds Media Group marehemu Ruge Mutahaba.
Mbunge wa jimbo la Nyamagana, mkoani Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula akisalimiana na mbunge wa Kigoma mjini Mhe. Zitto Kabwe baada ya kuwasili katika viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba asubuhi hii kumuaga aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi Clouds Media Group marehemu Ruge Mutahaba.
Mbunge wa jimbo la Nyamagana, mkoani Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula akimpa pole mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga katika viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba asubuhi hii katika ibada ya kumuaga aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi Clouds Media Group marehemu Ruge Mutahaba.
Comments
Post a Comment