Naibu Waziri Mkuu wa Algeria Ramtane Lamamra amesema kuwa serikali ya nchi hiyo iko tayari kufanya mazungumzo na upinzani, baada ya Rais Abdelaziz Bouteflika kuubatilisha uamuzi wake wa kutaka kugombea uchaguzi kwa muhula wa tano kutokana na maandamano ya umma.
Lamamra ameiambia redio ya taifa kuwa lengo la serikali ni kuwaleta pamoja Waalgeria wote.
Awali, Mkuu wa majeshi na naibu waziri wa ulinzi Ahmed Gaed Salah aliiambia televisheni moja nchini humo kuwa jeshi litalinda usalama wa Algeria katika mazingira yoyote yale.
Mpango wa Bouteflika ambaye ameahirisha uchaguzi na kusema kuwa kongamano litaangaliwa ili kujadili mabadiliko ya kisiasa, umeshindwa kuwaridhisha Waalgeria wengi ambao wanaendelea kushinikiza mfumo wa kisiasa wa nchi hiyo ulioduma uondolewe.
Comments
Post a Comment