RC Makonda amkingia kifua R. Kelly ishu ya unyanyasaji wanawake kingono, amtolea mfano Diamond

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda ameamua kuweka wazi hisia zake juu ya sakata la unyanyasaji wanawake kingono linalomkabili nguli wa muziki wa RnB duniani, R. Kelly.


RC Makonda amesema kuwa haamini tuhuma hizo kama ni za kweli, kwani kuna mastaa kibao ambao walishawahi kutuhumiwa kesi za namna hiyo na baadae wakashinda.

“Kuna Jambo limejificha hapa. Natamani tumsikilize tena R kelly. Inawezekana akawa mkweli, kwani wote hapo pichani wamewahi kupewa kesi za aina moja na mwisho jamii ikawaona kama wamechanganyikiwa. “ameeleza Makonda kwenye ukurasa wake wa Instagram na kumtolea mfano Diamond.

“Hivi kesho unaweza kutuambia kuwa @diamondplatnumzanawabaka wasichana na kuwafungia madale kweli? . Kwa sasa nimechagua upande wa R Kelly mpaka hapo baadae Mahakama itakapotoa hukumu, kwani Kwa sasa bado ni tuhuma.”

R. Kelly kwa sasa yupo nje kwa dhamana na bado upepelezi wa tuhuma za unyanyasaji kingono wanawake unaendelea.

Comments