Moto wateketeza chumba ndani ya Uwanja wa ndege Dar, Jeshi la zimamoto lazungumza kuhusu ajali hiyo

Imeripotiwa kuwa chumba kimoja cha ofisi kilichopo ndani ya jengo la Uwanja wa Ndege  wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNIA) kwenye  jengo la Terminal 3, kimeungua kwa moto ambao bado chanzo hakijajulikana.
Image result for airport Dar

Akidhibitisha taarifa hizo, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto JNIA, Maria Kulaya amesema kuwa, tukio hilo lilitokea jana jioni baada ya moto huo kuzuka ghafla katika chumba cha ofisi hiyo kinachotumiwa na wakandarasi.

Kulaya  akiongea na gazeti la Mwananchi, amesema ingawa moto huo haukuwa na madhara kwa vile jeshi hilo liliwahi baada ya kupewa taarifa, lakini baadhi ya nyaraka zilizokuwemo kwenye chumba hicho zimeteketea kwa moto.

Hata hivyo, bado chanzo cha moto huo hakijajulikana, “Kamishna Jeneral wa Zimamoto, Tobias Andengenye alitembelea leo hapa na tayari tumeshaanza uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto huu. Tutoa taarifa rasmi baada ya kukamilika kwa mchakato huu,”amesema ameeleza Kulaya.

Comments