KAGERE WA BIL 1 ATIKISA AFRIKA


KUNA uwezekano mkubwa mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere akaibuka mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu ambao Simba imegoma kumuuza kwa Sh.Bilioni moja kwa Zamalek ya Misri.

 Image result for picha za meddie kagere
Kagere amekuwa mshambuliaji mahiri kwenye michuano hii akiwa hadi sasa ameshapachika mabao sita, lakini yupo nyuma ya Moataz Al-Mehdi wa Al Nasri kwa bao moja, Al Nasri ilishaondolewa kwenye michuano hiyo.

Hii ina maana kuwa kama Kagere atafunga mabao mawili kwenye mchezo wa AS Vita atafikisha mabao nane ambayo Moataz hawezi kuyafikia na anaweza kuwa na upinzani kutoka kwa JeanMarc Makusu Mundele wa Vita Club ambaye ana mabao matano.

Hii ina maana kuwa pamoja na mashabiki kuutazama kwa jicho kali mchezo kati ya Simba na Vita Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Taifa, pia kutakuwa na vita ya wawili hao ya kuwania kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo mikubwa Afrika.

Kama Simba wakishinda, Kagere atakuwa kileleni kwa kuwa Vita wataondoka kwenye michuano hiyo moja kwa moja na Makusu atakuwa amebaki na mabao yake matano. Ukiachana na staa huyo wa Congo mpinzani mwingine wa Kagere ni Themba Zwane wa Mamelodi Sundowns ambaye ana mabao matano pia, lakini mchezaji anayefuata hapo pia anatoka Simba ambaye ni Clatous Chama ambaye ana mabao manne.

Comments