Mwimbaji mkongwe Jennifer Lopez(50) amevalishwa pete ya uchumba na mpenzi wake Alex Rodriguez(44) ambaye ni mchezaji baseball wa zamani siku ya Jumamosi March 9,2019 ikiwa ni baada ya kuwa kwenye ndoa kwa takribani miaka miwili sasa.
Kupitia ukurasa wa instagram wa Jlo amepost picha ikimuonyesha akiwa amevaa pete hiyo na kuweka caption yenye emoji za kopa huku mpenzi wake Alex Rodriguez aliandika “Amesema ndio” akiwa amepost picha sawa na ya mpenzi wake kupitia ukurasa wake wa instagram.
Jennifer Lopez ambaye tayari amepitia ndoa tatu tangu mwaka 1997, inaelezwa kuwa alianza mahusiano na Alex mwezi February 2017 na tayari Jlo ana watoto wawili aliozaa na mwimbaji Marc Anthony na kuelezwa kuwa Jlo amejihusisha kwenye mahusiano ya kimapenzi na jumla ya wanaume kumi na moja mpaka sasa.
Comments
Post a Comment